Wednesday, 28 August 2013

SABABU ZA AUNT EZEKIEL KUJERUHIWA MKONONI CLUB BILLICANAS JUZI.

REJEA TAHARIFA TULIYOIRIPOTI JANA JUU YA KUUMIZWA VIBAYA SEHEMU YA MKONO WA KUSHOTO,MSANII MAHIRI WA KIKE KATIKA TASNIA YA FILAMU NCHINI BIBIE AUNT EZEKIEL,KATIKA UFUATILIAJI WA KARIBU JUU YA TUKIO HILI,NI KUWA KILICHOTUMIKA KUMJERUHI BIBIE AUNT EZEKIEL NI CHUPA NA WALA SI KISU KAMA TULIVYORIPOTI AWALI,MHUSIKA AKIWA NI MSICHANA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA YVON BIGIRWA.
YVON BIGIRWA.
CHANZO CHA SAKATA ZIMA KINAELEZWA KUWA NI MAPENZI KAMA TULIVYOLENGA AWALI KUTOKANA NA MAONI YA WENGI,ILA UKWELI JUU YA HILI KAMA CHANZO CHETU KILIVYORIPOTI,SAKATA ZIMA LILISABABISHWA NA KUMGOMBANIA JAMAA MMOJA,AMBAYE CHANZO KINAZIDI KUELEZA KUWA HUYO JAMAA MWENYEWE PIA NI MUME WA MTU,TENA ALIYE NDANI YA NDOA YAKE,JAMAA ANAYEJULIKANA KWA JINA LA SUNDAY.
TIFU ZIMA LILIANZA MUDA MFUPI BAADA YA JAMAA HUYO KUINGIA UKUMBINI HAPO{CLUB BILLICANAS}SIKU AMBAYO SWAHIBA WAKE AUNT EZEKIEL,BIBIE WEMA SEPETU ALIKUWA AKIFANYA UTAMBULISHO WA WASANII WAWILI "MIRROR & ASALI" WASANII ANAOWASIMAMIA KAZI ZAO KUPITIA KAMPUNI YAKE YA ENDLESS FAME.
SUNDAY ALIPOINGIA UKUMBINI HAPO NDIPO AUNT EZEKIEL NA YVON WALIPOANZISHA TIFU,BAADA YA KILA MMOJA KUHITAJI KUWA NA SUNDAY KWA MADAI YA UHALALI BINAFSI,NDIPO VUTA NIKUVUTE HIYO ILIPOISHIA KWA AUNT EZEKIEL KUPIGWA CHUPA KWENYE MKONO WAKE WA KUSHOTO,NAKUKIMBIZWA HOSPITALI KWA MATIBABU.
HALI YA MWANADADA AUNT EZEKIEL KWA SASA INAENDELEA VIZURI NA TAYARI AMESHARUHUSIWA HOSPITALINI,AKIENDELEA KUUGUZWA NYUMBANI.
AUNT EZEKIEL


No comments: