Friday, 30 August 2013

SHOW YA UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA DIAMOND YAWAKUTANISHA KWA MARA YA KWANZA MADAM RITHA NA NEY WAMITEGO.

KWA MARA YA KWANZA JANA MSANII NEY WAMITEGO a.k.a TRU BOY ALIKUTANA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA BENCHMARK MADAM RITHA KWENYE SHOW YA UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA MSANII DIAMOND PLATNUMZ JANA KWENYE HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM,IKUMBUKWE AWALI MSANII NEY ALIIMBA BAADHI YA HISIA ZAKE KWENYE SINGLE YAKE MPYA INAYOFANYA VIZURI HIVI SASA "SALAAM ZAO"MISTARI INAYOLENGA JUU YA SHINDANO LA BONGO STAR SEARCH LINALOSIMAMIWA NA KAMPUNI YA BENCHMARK,ILIYOCHINI YA MADAM RITHA AKIDAI KUWA ZAWADI ZINAZOTOLEWA NA KAMPUNI SIYO SAHIHI NA BADALA YAKE NI MAGUMASHI,JAMBO LILILORIPOTIWA NA VYOMBO VINGI VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII TOFAUTI TOFAUTI KUWA MADAM RITHA AMEAHIDI KUCHUKUA HATUA YA KUMSHITAKI NEY WAMITEGO,JAMBO LILILOKUJA KUKANUSHWA VIKALI NA MADAM RITHA MWENYEWE AKIDAI HANA MPANGO HUO NA WALA HAFIKIRII KUFANYA HIVYO AKIHOFIA KUPOTEZA MUDA WAKE KWANI MSANII NEY HANA UWEZO WA KUMLIPA NA KAMA ILIVYO MUDA HAUKUSUBIRI,HICHO NDICHO KINACHOMFANYA KUOGOPA KUPOTEZA MUDA WAKE KWA JAMBO LITAKALO MCOST KWA KUUPOTEZA MUDA WAKE,SASA JANA NDIYO SIKU YA KWANZA ILIYOWAKUTANISHA WAWILI HAO BAADA YA MADAM RITHA KUKIRI KWENYE INTERVIEW YAKE YA AWALI WIKI KADHAA NYUMA ,JUU YA HILI KUDAI HAMFAHAMU WALA HAJAWAHI KUKUTANA NA NEY WAMITEGO,JAPO ALIENDELEA KUSISITIZA KUWA HANA KINYONGO NAYE NA ILE ANAICHUKULIA KAMA CHALLENGE KWAKE,NA KUIONA KAMA NI STYLE YA KWAKE {NEY}
ANAYOAMINI ITAMTOA ZAIDI KATIKA KAZI YAKE YA KISANII,HIZI HAPA BAADHI YA PICHA WALIZOPIGA NEY WAMITEGO NA MADAM RITHA WOTE WAKIWA RED CARPET MUDA MFUPI BAADA YA KUKUTANA KWA MARA YA KWANZA JANA.


No comments: