Wednesday, 19 February 2014

MANCHESTER CITY YABANANISHWA KWAO.

Matumani ya timu ya Manchester City kunyakuwa taji la ligi ya mabingwa ulaya yalipata pigo baada ya wachezaji wa Barcelona Lionel Messi na Dani Alves kuifungia timu yao ya Barcelona jumla ya mabao mawili katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Etihad Jana.
Messi alikuwa wa kwanza kufunga kupitia penalty katika dakika ya 54 alipoangushwa na difenda Martin Demichelis{Manchester City} aliyepewa kadi nyekundu na kutolewa nje ya uwanja.
Licha ya Manchester City kuwa kasoro mchezaji mmoja walijizatiti kukabiliana na timu hiyo ya Barcelona tokea Uhispania ila Dani Alves alizima matumaini yao mbele ya mashabiki wao alipofunga bao la pili mwisho mwisho wa kipindi cha pili.
Ili kuingia robo fainali Manchester City itahithitajika kuichapa Bercalona mabao matatu kwa bila.
Hizi ni baadhi ya picha zilizopigwa kwenye mechi hiyo iliyochezwa jijini Manchester kwenye uwanja wa Etihad Stadium,













NB>>>HII NI VIDEO INAYOONYESHA JINSI MAGOLI MAWILI YA FC BARCELONA YALIVYOFUNGWA

Katika mechi nyingine ya timu hizo kumi na sita, nchini Ujerumani Bayer Liverkusen iliicharazwa mabao manne kwa bila na Paris Saint Germain ya Ufaransa. Mabao matatu yalifungwa kipindi cha kwanza na la nne katika kipindi cha pili.
Leo Arsenal ambao wako katika nafasi ya pili kwenye ligi ya Uingereza itacheza dhidi ya bingwa mtetezi wa kombe hilo Beyern Munich wakati AC Millan ya Italia itakuwa ikipambana Atletico Madrid ya Uhispania.

No comments: