Saturday, 15 March 2014

BAADA YA NDOA YAKE KUVUNJIKA "NAAZIZI"AJIWEKA KWA PRODUCER HERRY SAPPY{HOME BOYZ PRODUCTION-KENYA}

Producer Herry Sappy & Nazizi.
Hivi karibuni, mwanahip hop wa kike na mmoja wa waasisi wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Nazizi, alithibitisha kuwa ameachana ma mume wake raia wa Tanzania, Vinny, na wapo katika harakati za kupeana talaka, Nazizi na Vinny mpaka sasa wana mtoto mmoja wa kiume. Pia Msanii huyo, ambaye ni member wa kundi la hip hop la Necessary Noize la nchini Kenya, inadaiwa  amekufa tena kimapenzi kwa Mtanzania mwingine ,ambaye ni producer Herry Sappy, anayefanya shughuli zake za kimuziki kwenye studio za Home Boyz Productions za nchini Kenya. Kwa mujibu wa bongo5.com, Nazizi amethibitisha kuwa na uhusiano na Herry Sappy tangu Valentine’s Day, Februari 14 mwaka huu{2014}, na uhusiano wao ni wa dhati kabisa.
Producer Herry Sappy,Mtoto Wa Nazizi & Nazizi Mwenyewe.
Aliyekuwa mume wa Nazizi{Vinny} & Nazizi enzi za Mapenzi yao.

No comments: