Taarifa zilizokuwa zikisika Chini kwa chini mtaani kuwa Msanii Mr Blue kwa sasa anatumia Madawa ya Kulevya,Madawa
Ambayo yanayomsababisha Kupungua kwa Ufanisi wake wa Kufanya Kazi na Hata
Kubadilisha Muonekano wake na Kuwa tofauti kabisa na Alivyokuwa awali.
Kupitia Kipindi cha TV katika Channel moja maarufu jijini msanii Nyandu Tozi alipokuwa akiizindua Video ya wimbo wake Mpya Ambao unajulikana kwa jina la MAMBO MENGINE BAADAE ambao pia amemshirikisha Mr Blue katika Chorus.
Ikiwa Kama ni Mfuatiliaji wa karibu wa Muziki Bongo Flava, Basi utakua unajua kuwa Mr Blue na Nyandu Tozi
ni Marafiki wa Karibu sana , Kutokana na urafiki na Ukaribu
waliokuwanao basi ni rahisi kujua jambo lolote ambalo linaendelea kwa
Rafiki yake, Kufuatia hilo Nyandu Tozi alipoulizwa kuhusu Mr Blue kutumia Madawa ya Kulevya Alijibu kama ifuatavyo...
"Unajua Mafans wanashindwa Kutofautisha, kuwa kwa sasa Mr Blue
anafanya maisha yake na ana Mtoto hivyo kwa sasa yeye ni Baba hawezi
kufanya Mambo kama aliyokuwa akifanya Zamani, Yule ni mwanangu na Vile
vitu hatumii kabisa ni mfumo tu wa maisha ameamua kubadilika"alifunguka NYANDU TOZ.

No comments:
Post a Comment