Thursday, 3 July 2014

EZDEN JUMANNE AFUNGUKA SABABU ZA KUVUNJIKA KWA NDOA YAKE NA DIDA

SIKU chache baada ya kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’, aliyekuwa mumewe, Mtangazaji wa TV1, Ezden Jumanne ameibuka na kutoa sababu kuu tatu za kutengena kwao, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
DIDA & EZDEN ENZI ZA MAPENZI MOTO.
Akizungumza na waandishi wetu katika nyumba aliyohamia kwa sasa, Kijitonyama, Dar, Ezden alisema mgogoro kati yake na Dida ulianza zamani ambapo Dida alikuwa na tabia ya kurudi usiku mnene, Ezden alidai kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, tabia hiyo ilizidi kuonekana ingawa alikuwa akimuonya mara kwa mara.
BIG BROTHER NDIYO TATIZO

Pamoja na sababu hizo, Ezden aliitaja sababu kuu iliyoanza kuzua mgogoro uliosababisha kuvunjika kwa ndoa hiyo ni Shindano la Big Brother Africa linalotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.
DIDA & EZDEN KATIKA SIKU YA HARUSI YAO,PEMBENI YAO NI SAUDA MWILIMA.
Alisema siku moja mtalaka wake huyo alimweleza kuwa kuna rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Furaha amempa mchongo wa kuwa mgeni staa (celebrity guest) ndani ya Jumba la Big Brother na kumuomba ampe ridhaa ya kwenda huko.
Source-Gpl.
 

 

No comments: