Thursday, 3 July 2014

WATANGAZAJI B12,Dj FETTY & ADAM MCHOMVU WAFUNGUKA JUU YA TUKIO LA WAO KUPIGANA STUDIO JANA.

ADAM MCHOMVU,B12 & Dj FETTY.
Kama ulikuwa Hewani siku ya jana katika kipindi maarufu kabisa (XXL), ndani ya Station maarufu hapa Tz  CLOUDS Fm utaelewa nini ninachotaka kukizungumzia mpaka sasa. Katika hali isiyotegemewa jana watangazaji watatu maarufu , DJ FETTY, ADAM MCHOVU na B12 walizichapa ndani ya studio za Clouds live huku wakisahau kuwa Wasikilizaji wanawasikia mwanzo mwisho wanachokifanya huko ndani ya studio. Sakata hilo lililosababishwa  na kutoelewana baina yao  juu ya mauzo ya Albam ya Fiesta! 
Sakata hilo lilisababisha mambo mengi kuzungumziwa  huku wengine wakijaribu kuliongelea kama ni jinsi ya kutafuta Tension{KEEK} kwa wasikilizaji,wakidai kuwa watu wengi Kwa sasa wamekuwa wakiacha kusikiliza kipindi hicho na kuhisi kupoteza UBORA uliokuwepo awali.
TASWIRA BAADA YA TIMBWILI NDANI YA STUDIO ZA CLOUDS FM JANA.

 
Sasa leo watu mbalimbali na wasikilizaji walikuwa wanataka kujua nini zaidi kilitokea kupitia kipindi cha Hekaheka, chanzo cha ugomvi hasa ni nn?
Baada ya massage nyingi sana kwenye kipindi cha hekaheka ilibidi wahusika wanyanyue simu zao kuwatafuta Adam, Fetty na B12 kujua nini kilichosababisha kuchapana makonde wakati bado kipindi kikiwa hewani. Muhusika alinyanyua moja kwamoja simu na kumpigia B12 ambaye alikataa kabisa kueleza chanzo cha sakata hilo la kutwangana huku akisema mambo yote yapo kwa uongozi.....

No comments: