Saturday, 30 August 2014

KESI YA KAYUMBA NYAMWASA: WANNE HATIANI KWA JARIBIO LA MAUAJI AFRIKA KUSINI

*Watanzania watatu hatiani, Mnyarwanda mmoja
*Wawili waachiwa huru

Watu wanne wamekutwa na hatia ya kujaribu kumuua mkuu wa zamani wa jeshi la Rwanda, Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa, nchini Afrika Kusini mwaka 2010. Washukiwa wengine wawili, akiwemo aliyedaiwa kuwa kinara wa genge hilo na dereva wa zamani wa Nyamwasa, wameachiliwa huru. Jenerali Nyamwasa alipigwa risasi na kujeruhiwa nje ya nyumba yake mjini Johannesburg.
 Alikwenda kuishi Afrika Kusini miezi kadhaa mapema kabla ya kufarakana na mshirika wake wa zamani, Rais wa Rwanda Paul Kagame. Akitoa hukumu, hakimu amesema ameridhishwa na ushahidi kuwa mshukiwa Hemedi Dendengo Sefu, raia wa Tanzania, ndio alifyatua risasi, huku Amani Uriwane, raia wa Rwanda na Hassan Mohammedi Nduli na Sady Abdou- wote raia wa Tanzania, walikuwa wakishirikiana naye. Rwanda imekanusha kuhusika na shambulio hilo. Hukumu itatolewa Septema 10.

No comments: