![]() |
| Afande Sele |
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya nchini Seleman Msindi ‘Afande Sele’, juzi kati alinaswa akiwa na demu mpya ikiwa ni siku moja tu baada ya kufanyika kwa 40 ya aliyekuwa mzazi mwenzake, marehemu mama Tunda. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Septemba 21 mwaka huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati staa huyo aliyekuwa mmoja wa watoa burudani katika tamasha la Fiesta, alipoonekana akiingia akiwa ameambatana na mrembo mmoja akiwa ameshikana naye kimahaba. Akiwa ndani ya uwanja huo, mkali huyo wa mashairi yenye vina kwa muda mwingi alikuwa pamoja na msichana huyo ambaye hakufahamika jina, wakiwa na dalili zote za wapendanao.
![]() |
| PICHA-Afande Sele na Binti huyo. |


No comments:
Post a Comment