Tuesday, 4 November 2014

EMMANUEL MBASHA AUKWAA MSALA MWINGINE"NI JUU YA UTATA JUU YA KIFO CHA MFANYAKAZI WAKE ALIYEJINYONGA NYUMBANI KWAKE"


Majanga yanazidi kumuandama aliyekua mume wa muimbaji maarufu wa muziki wa Injili nchini Bi,Frola Mbasha, akiwa bado ana kesi mahakamani akidaiwa kumbaka ndugu yake mkewe,
Na hili ndilo janga jingine lilimkuta Emmanuel Mbasha. Janga hilo ni la kufariki kwa mfanyakazi wake wa ndani ambaye alijinyonga ijumaa iliyopita. Inadaiwa kuwa Emmanuel na mfanyakazi huyo walikua wakiishi wawili tu ndani ya nyumba ya Emmanuel, lakini kitu cha kushangaza zaidi ni pale mfanyakazi huyo alipojinyonga. Inavyosemekana Emmanuel hakutoa taarifa kwa majirani kuhusu tukio hilo badala yake alitoa taarifa polisi na kisha kuusafirisha mwili wa marehemu kwa siri sana kwenda kumzika Singida.
Tumepata ujumbe kutoka kwa mmoja wa majirani wa Emmanuel Mbasha ambaye hakutaka jina lake litajwe, ujumbe huo ulisema ” Kuna kijana wa kazi toka Singida alikuwa anaishi na Emmanuel Mbasha, amejinyonga na kuacha ujumbe kuwa kwa yaliyomkuta ameamua bora ajinyonge. Walikuwa wanaishi na Mbasha tu huko ndani na baada ya kujinyonga Mbasha amefanya siri kubwa mno hawakuweka hata msiba. Kijana alijinyonga Ijumaa na ndugu wakatafutwa wakaenda kureport polisi kwa ajili ya mazishi na wamemsafirisha kwenda kuzika Singinda. Mbasha hakutaka majirani tujue. Mnaweza kumtafuta kwa maelezo zaidi maana nikiandika hapa yeye ndiye mwenye ukweli alimfanyia nini kijana wa watu.”Alidai jirani mmojawapo.

No comments: