Friday, 6 March 2015

TAMBO ZA KIGOGO IKULU ZAWACHEFUA WATANZANIA

Kauli ya Mnikulu, Shaban Gurumo, kwamba hata kama asingepata mgawo wa Sh. milioni 80.8 kutoka kwa mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, James Rugemalira, angeweza kutatua shida zake kwa kuwa anamiliki fedha zaidi ya hizo, imeelezwa kuwa ni ya dharau, kuudhi na pia ni kejeli kwa Watanzania, ambao wengi wao ni maskini.

KIJO-BISIMBA
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Utawala Bora (LHRC), Dk. Hellen Kijo-Bisimba, alisema kauli kama hizo zimekuwa zikitolewa kwa sababu wanaozitoa wanaona Watanzania ni watu wasioelewa kitu. “Wanasema hivyo, kwa sababu wanaona hakuna anayeweza kufanywa chochote,” alisema Dk. Bisimba.
Hata hivyo, alisema Gurumo na watu wengine mfano wake, wanapaswa kuulizwa wanakozitoa fedha hizo wakiwa watumishi wa umma.

DK. BANA
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema kauli za watu kama Gurumo, mbali ya kuwachanganya wananchi, ni za kuudhi. Alisema hiyo ni kutokana na ukweli kwamba, wamekuwa wakitoa kauli kama hizo bila kuzipima namna zitakavyopokelewa na kutafsiriwa na wananchi. “Watu wa kawaida wanaona ni kejeli. Kama unazo fedha nyingi ni zako. Kauli ya Gurumo haiakisi maadili mema, hasa kwa Watanzania maskini. Wanapokea kama ni dharau.” alisema Dk. Bana. Aliongeza: “Sijawahi kusikia kauli kama hii. Watanzania, ambao ni maskini wanategemea maadili mema kwa viongozi wao, hawaipokei kauli hiyo vizuri.”

Wewe kama mwananchi{Mtanzania} unaichukuliaje kauli hii ya bwana Gurumo?

TUTUMIE MAONI YAKO HAPA>>>>https://www.facebook.com/Ngessakinollo 

No comments: