Ni jioni ya Jumatano ya April 15 2015
nipo ofisini na naanza kupokea simu nyingi za watu wangu wakitaka kujua
ukweli kuhusu taarifa zilizoenea kwamba msanii wa bongofleva Hussein Machozi amefariki kwenye ajali iliyohusisha gari la mizigo na gari dogo Dodoma.
Baada ya hapo naanza kupiga simu ya Hussei Machozi
inaita lakini haipokelewi kwa zaidi ya nusu saa, naanza kupata
wasiwasi, nikiwatafuta rafiki zake pia sifanikiwi lakini baadae
naendelea kuipiga simu ya Hussein na inapokelewa.
Sauti ni ya Hussein mwenyewe, anaanza kwa kusema ‘Nilijiandaa
hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye
charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missedcalls nyingi sana,
msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga
simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali
na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipo Dar es salaam‘
Kumbe baada ya taarifa za kifo kusambaa na
kuwafikia Mama yake mzazi pamoja na dada yake ambao walipiga simu yake
na haikupokelewa kwa muda mrefu, wakaamini kweli kilichotokea ni kifo…. mama akazimia hapohapo, dada akaanguka na kuzimia vilevile.
Sasa hivi Hussein inabidi alazimike
kusafiri mpaka kwao Singida Manyoni ili kuwahakikishia ndugu zake kwamba
yuko hai manake aliongea kwenye simu ya kaka yake na kumpa Dada simu
baada ya kuzinduka lakini dada hajaamini, kasema anafichwa tu lakini ni kweli Hussein kafariki.
Mama anaendeleaje? ni yapi mengine ameyasema Hussein Machozi? bonyeza play hapa chini kumsikia mwenyewe…



No comments:
Post a Comment