Baada
ya kupitia kipindi kigumu cha misukosuko ya kusemwa na vilevile
kutukanwa mitandaoni na kulalamika sana, star wa muziki Linah Sanga
amesema kuwa bado ana dukuduku kubwa moyoni ambalo anajipanga hivi
karibuni kulianika hadharani kwa njia ya tamko rasmi ambalo atalitoa kwa
njia hiyo hiyo ya mtandao.
Kwa mujibu wa Linah kupitia mahojiano exlusive tuliyofanya naye, amesema kuwa tamko hilo kwa sehemu linahusiana na tuhuma za kulalamika kuibiwa bwana, kitu ambacho kinaendelea akiwa haoni sababu ya kuendelea kukaa kimya zaidi, na kuumia roho.
Linah amesema kuwa, kwa sasa anajipanga kuandaa waraka huu na kuanzia siku yoyote kutoka sasa, mambo yote kutoka moyoni mwa mrembo huyu anayetikisa chati za muziki ndani na nje ya Tanzania, yatakuwa hadharani.

No comments:
Post a Comment