Thursday, 11 June 2015

SABABU YA MUIGIZAJI ESHA BUHETI KUPIMA UKIMWI NA KUYAANIKA MAJIBU YAKE.

Esha Buheti.

Actress mkali kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Esha Buheti ameshare na fans pamoja na followers wake kupitia instagram majibu ya vipimo vyake alivyochukua baada ya kupima ugonjwa wa UKIMWI.
Esha ametumia “time” yake kuihasa jamii, kuhamasika kupima virusi vya UKIMWI akiwataka kuto ogopa kwa maana kila jibu litakalotoka kuna namna ya kuweza kuishi kwa kufuata taratibu ulizo pangiwa na wataalam.
Mwigizaji huyo amepost fomu ya majibu iliyodhihirisha hana virusi vya ukimwi(negative), na caption ambayo imefafanuliwa na wazee wa ubuyu kuwa mwenzi wake “alichepuka” na baada ya Esha kupewa taarifa ndipo alipoamua kwenda kupima. “Kupima sio Kazi Kazi Ni kuchukua majibu…., y tumekua waoga sana kupima? Nahisi Ni vzr kuijua afya yako….. Haimaanishi kama ukikutwa na HIV Ndo mwisho wa maisha yako kwa upande Wangu mm hakuna ugonjwa nauogopa kama cancer……
 Jana nlipoenda kupima nilikutana na mwandishi wa habari na nikamwambia nipo tayari kwa jibu lolote alinihoji y nimekua jasiri sana! Kiukweli kupokea majibu kunahitaji ujasiri….. Na nilimwambia kama nitakuwa ninao naomba niwe msanii wa kwanza kujitangaza……. Kuna habari mbaya sana nilizipokea ikanibidi niende kupima majibu yalipotoka sikuamini wallah mungu ananipigania sana Nasitaacha kumtumainia…. Ushaurii tuuu Ni vizuri kujua afya zetu coz hakuna anayejua nyendo za mwenzi wake…… Team amasisha#wengine# Tanzania bila ukimwi inawezekana” ameandika Esha. Tazama karatasi yake ya majibu hapo chini.

No comments: