![]() |
| Mwanamuziki wa Dansi nchini Ramadhan Masanja"Banza Stone"akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Manispaa Kinondoni{Mwananyamala Hospitali} |
Ijumaa Wikienda lilitia maguu kwenye hospitali hiyo na kufanikiwa kumuona Banza ambaye kwa wakati huo alikuwa amezungukwa na watu mbalimbali, wakiwemo wanamuziki wenzake wa dansi wengi wakiwa ni wale wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Kila aliyekuwa akimuona mwanamuziki huyo aliyekuwa akibamba vilivyo kila alipopanda jukwaani, alikuwa akihuzunika huku wasanii wenzake wakiangua vilio kutokana na kutoamini alivyo Banza kwa sasa.
![]() |
| Banza akipewa kikombe cha uji. |
Naye kaka wa Banza, Hamis Masanja alisema waliamua kumpeleka hospitali kutokana na hali yake kuwa mbaya ambapo Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, Asha Baraka akiwa na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) walifika nyumbani kwa ajili ya kumjulia hali ndipo wakaafikiana kumpeleka hospitali.
Kwa muda mrefu Banza amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi za kichwani hali iliyomsababishia matatizo ya kutosikia na kutoona vizuri huku akishindwa kabisa kunyanyuka kitandani.
![]() |
| Banza Stone wakati akiwa na afya yake. |




No comments:
Post a Comment