![]() |
| ACP David Misime. |
Imeandikwa kwenye Magazeti mengi leo
July 07 2015 kwamba kama huna shughuli ya kufanya Dodoma, na ulijipanga
kwa ajili ya safari ya kwenda huko basi ni bora ukaahirisha ili kuepuka
usumbufu.
Ninazo sentensi za Kamanda wa Polisi Dodoma akiagiza haya >>> “Tunaomba kila mmoja atambue na kila mara akumbuke kwamba Ulinzi na Usalama unaanza na yeye mwenyewe kwanza” >>>
“Jeshi la
Polisi linashauri wale wote ambao wanataka kuja Dodoma wiki hii, kama
huna shughuli maalum inayomlazimu kuja ni vizuri wasije ili kuepuka
usumbufu… Wengine wanaweza wakaja kwa lengo la kushuhudia kinachoendelea
au ushabiki tu… Wawaweza wakakosa mahali pa kulala” >>>- ACP David Misime.
Kuna matukio makubwa mawili ndani ya Dodoma wiki hii, Rais JK atavunja
Bunge ambalo lilikuwa kwenye Kikao cha Bajeti pamoja na kupitisha
Miswada mbalimbali, kingine ni Chama cha CCM kupitisha jina la Mgombea
wa Urais kati ya Makada zaidi ya 35 waliojitokeza.
NB:-MSIKILIZE HAPO CHINI,

No comments:
Post a Comment