Wednesday, 8 July 2015

Diamond Platnumz na Producer Manecky wamaliza tofauti zao.

Diamond Platnumz.
Producer Manecky wa "Am Records"na msanii mahiri wa Bongo Fleva Diamond Platnumz waliowahi kuripotiwa kuwa na tofauti baada ya Diamond Platnumz kuacha kurekodi kwenye studio za Am Reocrds na Producer Maneck kwa madai kwamba Manecky alikuwa akivujisha nyimbo zake. wamemaliza tofauti zao.
Kuonyesha hali ya kupatikana suluhu kati yao,Manecky aliweka picha yake na Diamond wakiwa pamoja kwenye studio yake ya Am Records akiambatanisha Picha hiyo na ujumbe wa kusamehana, kwa mujibu wa post yake imeonekana ni meneja wa Diamond Platnumz ndiye aliyefanikisha kumalizika kwa mzozo huo. Haya ndiyo maneno yanayosomeka kwenye post yake
Kwa Mara nyingine Tena”In life tujifunze kusamehe na kusahau hakuna ajuae Kesho#aboutLast9te#Ramadankareem #AmRecordsHoMeGoodMusic 
UNAJUA VILE TUNAFANYAGA WHEN MOND meets NeCk..
I missed workin with him Sasaaa Basii… @babutale ubarikiwe Boss


HII HAPA NI CLIP INAYOMUONYESHA PRODUCER MANECKY WA AM RECORDS AKILIONGELEA HILO NA NINI KITAFUATA BAADA YA WAO KUPATANA,

No comments: