Mshindi wa project ya Airtel Trace Music Star kutoka Tanzania ambaye
pia ndiye muwakilishi wa bara la Afrika Mayunga Nalimi amesimama kwa muda
kuendelea na project hiyo baada ya Mwanamuziki Akon msimamizi wa
kumsaidia kijana huyo kufanya yake ikiwemo suala la kurekodi nyimbo ,
kuomba muda kidogo kumalizia mambo yake.
“Ni kweli nilitakiwa kwenda Marekani na kukutana na Akon, lakini mambo yameingiliana kidogo sababu Akon anamalizia project yake ya kusambaza umeme kwa baadhi ya sehemu Afrika, hivyo ameomba muda amalizane na hizo mambo kisha ataendelea na mimi”, alisema Mayunga wakati akifanyiwa mahojiano ndani ya kipindi cha Morning Trumpet cha Azam TV.
Kutokana na hilo basi Mayunga ameona kuliko kukaa kimya huku akimsubiri Akon, ameamua kutoa wimbo wake aliourekodi chini ya producer Man Walter, wimbo ukiitwa “Nice Couple” ambao umeandikwa na Producer huyo kutoka studio ya Combination Sound.
Mayunga amesema Video ya wimbo “Nice Couple” imefanyika nchini Afrika Kusini maeneo ya Soweto, ikiwa imepata Baraka zote toka kwa kampuni ya Airtel na kuomba watanzania waipokee hiyo kwanza kisha wawe wavumilivu kwani mambo mazuri yanakuja.

No comments:
Post a Comment