Staa mkongwe wa muziki kutoka DR Congo, Jenerali Defao baada ya
kutosikika kwa muda mrefu ameonekana huko Kenya, akiwa na muonekano
tofauti na alivyozoeleka kutokana na kupungua mwili kwa kiasi kikubwa,
na weupe wa ngozi yake ukitia mashaka.
Defao
ambaye hata hivyo haijajulikana rasmi ni shughuli gani imempeleka huko
Kenya, kutokana na muonekano huo, hisia za wengi zimetafsiri kuyumba
kisanaa na kiafya kwa msanii huyo aliyewahi kuwa gumzo kwa sanaa yake
katika bara la Afrika na Ulaya.
Hata hivyo, kuyumba kwa msanii huyo pia kunahusisha na kupungua kwa mvuto wa aina ya muziki wa dansi kutoka DR Congo ambao ulifanya vizuri sana katika miaka ya nyuma.
Hata hivyo, kuyumba kwa msanii huyo pia kunahusisha na kupungua kwa mvuto wa aina ya muziki wa dansi kutoka DR Congo ambao ulifanya vizuri sana katika miaka ya nyuma.

No comments:
Post a Comment