Monday, 28 September 2015

PEPO LA UDHALILISHAJI LAMGANDA JUMA NYOSSO.

Mchezaji wa Mbeya City, Juma Nyosso aliyewahi kufungiwa na TFF mechi 8 kwa kumdhalilisha mchezaji mwenzake, amerudia tena na Kwakumdhalilisha mchezaji mwenzie John Bocco wa Azam FC

-Tukio hilo lilitokea kwenye mechi ya Azam FC na Mbeya City.....


BEKI huyu kisiki wa klabu ya Mbeya City Juma Nyoso aliwahi kufungiwa na Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) kwa kosa la kumfanyia vitendo kama hivi vya udhalilishaji aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Elius Maguri.
Baada ya adhabu hiyo jamii ya wanamichezo iliamini kuwa Nyoso amejifunza kitu na kwavile alijitokeza kumtaka radhi Maguri basi ilitarajiwa asingerudia tena kutenda kosa hilo.
Jioni ya jana katika mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom kati ya Azam na Mbeya City Nyoso amethibitisha utukutu wake na kwamba ile ya kwanza haikuwa kwa bahati mbaya. Kwa mara nyingine amerudia kufanya kitendo kile kile cha udhalilishaji na safari hii akimfanyia mshambuliaji wa Azam John Bocco.
Kitendo hicho kimenaswa na kamera zilizokuwepo uwanjani hapo na ni matumaini ya wapenda soka kuwa TFF itachukua hatua kali zaidi za kisheria kwa Nyoso ili iwe fundisho kwake na kwa wachezaji wengine ambao wanafanya vitendo hivi.

No comments: