![]() |
Mwigizaji Kingwendu ni
miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao walichukua headlines za kugombea
ubunge kwenye uchaguzi mkuu 2015 ambapo wengine ni pamoja na Afande Sele, Professor Jay na Mwigizaji Frank.
Mwigizaji/Mchekeshaji
Kingwendu hakufanikiwa kushinda kwenye kura za ubunge huku tiketi yake
kulitaka Bunge ikiwa inapitia CUF jimboni Kisarawe mkoa wa Pwani.
Baada ya kushindwa, Kingwendu ameongea na kusema yafuatayo >>> ‘Kiukweli
kabisa matokeo ya mwanzo kabisa ilikua inaonyesha mimi naongoza lakini
baada ya kumaliza kuhesabu kura ikaonekana amenishinda yule bwana Suleiman Jafo wa CCM‘
‘Nimejaribu
na nimethubutu kwa mara ya kwanza kugombea nafasi kubwa ya Ubunge..
nimeenda vizuri tu na sitachoka na wala sitaacha, najipanga tena kwa
mara nyingine najua nimekosea wapi na ntajipanga upya na ntaenda kusomea
siasa zaidi‘– Kingwendu
‘Mwaka
2020 huko nadhani nitakua niko sawa, nakwenda kusomea siasa zaidi ili
niijue siasa zaidi na nijue nitamkamata wapi, kuhusu kushawishiwa
kuingia kwenye siasa, hakuna mtu aliyenishawishi kugombea ubunge bali ni
mimi mwenyewe niliamua baada ya kuona pia baadhi ya wasanii wenzangu
wanagombania kama nilivyomuona Mr. II Sugu kipindi kile‘-Kingwendu


No comments:
Post a Comment