Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa imeeleza kuwa hadi sasa wamepokea maombi mengi ya wasimamizi wa uchaguzi mkuu kutoka kwa nchi za ulaya kupitia umoja wao.
Miongoni mwa wasimamizi wa uchaguzi huo utakaofanyika oktoba 25 mwaka huu ni nchi za umoja wa jumuia ya madola zitakazoongozwa na Rais Mstaafu wa Nigeria Goodluck Jonathan, na kwa upande wa Afrika Union ameteuliwa rais mstaafu wa nchi ya Msumbiji Armando Guebuza. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, kaimu katibu mkuu balozi Yahaya Simba amesema mbali na makundi hayo ambayo yamelipa heshima swala hilo hapa nchini, pia nchi za kusini mwa jangwa la sahara zitatuma wasimamizi.
Aidha ameeleza pia sherehe za maadhimisho ya kuundwa kwa umoja wa mataifa ambao unafikisha miaka 70, zilizopangwa kufanyika oktoba 24, zimerudishwa nyuma hivyo inabidi zifanyike oktoba 15 kutokana na mchakato wa uchaguzi kuingiliana tarehe.
No comments:
Post a Comment