Thursday, 15 October 2015

MAGUFULI AMFAGILIA DIAMOND PLATINUMZ.

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amemmwagia sifa lukuki, mkali wao ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutokana na ushindi wa tuzo tatu za Afrimma zilizofanyika wikiendi iliyopita nchini Marekani

katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili mkoani Lindi baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba kushuka jukwaani kukamua kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais, ndipo Magufuli alishika kipaza sauti na kumsifia Diamond aliyeshinda tuzo za Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Msanii Bora wa Mwaka na Utumbuizaji Bora wa Video.
Mgombea Kiti cha Urais{CCM}Dkt,J.P.Magufuli
 

No comments: