Tuesday, 10 November 2015

RONALDO NA MAISHA YA UPWEKE.

Cristiano Ronaldo na Mwanae.

Mtayarishi wa sinema inayoangazia maisha ya mwanakandanda wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo anasema kuwa nyota huyo anaishi maisha ya upweke mno.
James Gay-Rees ambaye alipata umaarufu kwa kuandaa filamu kuhusu ya maisha ya mwendesha magari ya langalanga Senna, raia wa Brazil, anasema kuwa Christiano hana marafiki wengi.
" ana marafiki wachache mno''
''mara n
yingi Cristiano huwa na familia na jamaa zake'' alisema James.
Cristiano Ronaldo kwenye "Selfie"na Mamaake Mzazi.

''nafikiri kuwa kule kujituma kunamtaka awe na nidhamu ya hali ya juu mwenyewe. Hivyo analazimika kujinyima vitu vingi kiasi ambacho hakiaminiki katika macho ya mtu wa kawaida''.
Filamu hiyo imewalazimu james na kundi lake la wapiga picha wamekuwa wakirekodi kila kitu katika maisha ya Ronaldo kwa kipindi cha mwaka mmoja hivi.
Kilichomshangaza James ni unyenyekevu wa nyota huyo mshindi mara tatu wa tuzo la mchezaji bora duniani.

''Kwa hakika kuwa nyota wa hadhi kama yake inataka kuwa mnyenyekevu wa kupindukia'' alisema James.
James alikanusha dhana ya kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid na Ureno ni mjeuri sio kweli.

No comments: