Thursday, 19 November 2015

WASIFU WA WAZIRI MKUU MTEULE Bw,KASSIM MAJALIWA.

Bw,Kassim Majaliwa.

Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John P Magufuli, leo ametegua Kitendawili cha nani atakuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya 5 kwa kumteua Mh Kassim Majaliwa.
Kassim Majaliwa ni Mbunge aliyetokea katika Chama cha Mapinduzi CCM, akiwakilisha jimbo la Ruangwa Lililopo mkoani Lindi.
Mh Majaliwa kabla hajateuliwa kuwa Waziri mkuu alikuwa Naibu Waziri TAMISEMI. ‘Professional’ yake hasa ni mwalimu, aliwahi pia kuwa katibu wa Chama cha Walimu mkoa, mkuu wa Wilaya ya Singida na nyadhifa nyingine tele za kuwahudumia wananchi.
Kwa kiasi kikubwa baadhi ya Wabunge wakongwe wa Chama cha Mapinduzi, wameonyesha kuwa na imani na Mh Kassim Majaliwa.

WASIFU WA WAZIRI MKUU MTEULE WA SERIKALI YA AWAMU YA 5
Mh Kassim Majaliwa
1970 1976 Shule ya Msingi Mnacho cheti cha Elimu ya Msingi
1977 1980 Shule ya Sekondari Kigonsera CSEE
1991 1993 Chuo cha Ualimu Mtwara
1994 1998 Chuo kikuu cha Dar es Salaam, shahada ya kwanza
1999 1999 Chuo kikuu mjini Storckolm PGDP
2010 2014 - MB
2006 2010 PM Mkuu wa Wilaya
2001 2006 PS-CWJ Katibu Mkoa
2001 2001 PS-CWJ Katibu Wilaya
1988 2000 PS-Moec Mkufunzi
1984 1986 TD-Lindi Council Mwalimu

Amezaliwa December 22 mwaka 1960 na mpaka hivi sasa ana umri wa miaka 54, na ana Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

No comments: