Sunday, 21 February 2016

Meya Kinondoni: Makonda punguza Sifa, Fuata Taratibu.

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob adai Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda anaingilia majukumu ya Halmashauri ambayo sio ya kwake

-Amesema kuwa hakuna sheria inayomruhusu Makonda kushirikiana kikazi na Halmashauri hadi awasilishe barua ya maombi kwa Mkurugenzi ama Meya kama anahitaji kufanya jambo lolote.


Meya wa manispaa ya Kinondoni, Boniface amemuonya DC Makonda kwa tabia yake ya kuingilia kazi za halmashauri.

Meya huyo wa CHADEMA chini ya mwamvuli wa UKAWA,Amesema DC Makonda amekuwa akifanya kazi asizostahili kuzifanya ili tu apate sifa.Na kuzoa zoa vyombo vya habari.

Amemuasa awe kama wenzake waliomtangulia akitolea mfano wa Lukuvi,Makamba n.k amesema hawa ni watu waliyajua majukumu yao na mipaka yao ya ukuu wa wilaya. 

No comments: