Monday, 30 May 2016

WEMA AJIBU DISS YA HARMONIZE


Msanii wa kike wa Filamu Bongo Wema ‘Abraham’ Sepetu, amefunguka na kudai kuwa yeye hashtushwi na kauli ya Diss kutoka kwa mwanamuziki Harmonize kwa sababu ni miongoni kati ya changamoto za umaarufu.
Akizungumza kupitia kipindi cha kubamba cha Times Fm kinachoruka kila jumapili, Wema amedai kwa sasa anaangalia zaidi shughuli zake kuliko kusikiliza watu wanasema nini juu yake kwa kuwa ameshatukanwa matusi ya kila aina. “Me i dont want to talk about WCB man, its a price u pay for been famous Honey, kama huongelewi vibaya we sio star rais anaongelewa vibaya ntakuwa mimi?, am a very postive hawawezi ishiwa cha kuongea so u killn them with a Success” Alisema Wema.
Wiki iliyopita Harmonize mmiliki wa hit ‘Bado’ alionekana kwenye clip fupi ya video akirap kuwa ‘Sister du usitoe mimba kesho uliye ka Sepetu’ ambayo alidai ilikuwa ni maalum kwa ajili ya promo ya wimbo wa msanii mwenzie Raymond uitwao ‘Natafuta Kiki’.

No comments: