Friday, 30 August 2013

RAY C ACHUKUA UAMUZI WA KUMRUDIA MUNGU,AOKOKA NA KUBATIZWA,UBATIZO WA MAJI MENGI.

MSANII MAHIRI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA NCHINI ALIYEWAHI KUATHIRIKA NA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA,MPAKA KUFIKIA KUPATA MSAADA NA HURUMA YA MH,RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH JAKAYA MRISHO KIKWETE,KWA KUMLIPIA MATIBABU NA HUDUMA NYINGINE HADI KURUDIA HALI YAKE YA AWALI,
MSANII REHEMA CHALAMILA,a.k.a RAY C AMECHUKUA UAMUZI,ULIOONEKANA WA BUSARA MBELE YA WENGI NA WAKUYANUSURU MAISHA YAKE KWA UJUMLA,HII NI BAADA YA MWENYEWE KWA KINYWA CHAKE KUMKIRI KRISTO KAMA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKE,HII NI BAADA YA KUKUBALI KUONGOZWA SALA YA TOBA NA HATIMAYE KUOKOKA RASMI,IKIFUATIWA NA KUBATIZWA UBATIZO WA MAJI MENGI,
MAAMUZI HAYO KWA RAY C YALIFIKIWA KATIKA KANISA LA "THE POOL OF SILOAM INTERNATIONAL MINISTRY"KANISA LENYE MAKAO YAKE MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM,MAENEO YA MBEZI BEACH{MAKONDE},CHINI YA MTUME NA NABII ELIYA.
KUFUATIA UAMUZI WAKE HUO RAY C AMETUPIA PICHA ZENYE MAELEZO JUU YA UAMUZI WAKE HUO KUPITIA MTANDAO WA INSTAGRAM,AKIONYESHA KUTOJUTIA KABISA MAAMUZI YAKE HAYO ALIYOYAAMUA,AKIWA AMEAMBATANISHA MANENO"SHIKA NENO TENDA NENO"KWENYE PICHA ZAKE HIZO ALIZOTUMA MTANDAONI,
IKIWA NI SLOGAN YA WANA"SILOAM" MWANADADA RAY C AMEONYESHA KUITUMIA SLOGAN HIYO AKIONYESHA KUWA NA YEYE PIA NI MMOJA KATI YA WANA"SILOAM"KWA SASA,BLOG YETU INAMPONGEZA SANA RAY C KWA UAMUZI WAKE HUO WA KUMRUDIA MUNGU KATIKA MAISHA,MUNGU AMTIE NGUVU AMSAIDIE NA KUMBARIKI KATIKA KAZI ZAKE ZOTE.

No comments: