Friday, 9 January 2015

FLORA MVUNGI AFURAHIA KUWA NA MTOTO.

Flora Mvungi na Kabinti kake.
Muigizaji wa filamu hapa Bongo, Flora Mvungi ‘H-Mama’ ambaye ni mama wa mtoto mmoja, amewashinikiza wasanii wenzake wa kike kuzaa mapema huku akiwataka kuingia kwenye hatua ya kuitwa mama na kusema kuzaa kuna raha yake.
Akizungumza na mwandishi wa GPL, Flora alisema baadhi ya mastaa wamekuwa na dhana potofu kwamba, ukizaa unazeeka na utakuwa hufanyi starehe, jambo ambalo halina ukweli.
“Mimi nawashauri wazae tu, kuzaa kuna raha yake bwana. Unajua starehe haziishi, kikubwa ni wao kuzaa fasta kisha mambo mengine yanaendelea huku tayari wakiwa wameshaweka ile heshima ya kuitwa mama,” alisema Flora.
Flora Mvungi ni mke wa msanii HBABA ambapo Ndoa yao ilifungwa mwaka jana,kwa muongozo wa dini ya kiislam.

No comments: