Friday, 17 April 2015

WEMA SEPETU AKIRI KUIMBWA NA DIAMOND KWENYE WIMBO "NASEMA NAWE" ,ASISITIZA DIAMOND NI MSHAMBA!!


Staa wa filamu za kibongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amesema ni ushamba kwa wasanii wa muziki kuwatungia nyimbo za majungu wasichana wanaoachana nao kimapenzi. 
Wema amesema wasanii wengi wa muziki wamekuwa na tabia ya kishamba ya kutunga nyimbo zenye maneno ya kuudhi, wakiwalenga waliokuwa wapenzi wao. “Ni ushamba wa mapenzi, haiwezekani mlikuwa mnafurahia wote mapenzi yenu, lakini mkiachana anakutungia nyimbo za kukuponda, hakuna neno la kuzungumzia hilo zaidi ya kuita ushamba kwa wasanii wa aina hiyo,’’ alisema Wema. 
Hata hivyo, kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kutoka studio moja kubwa ya kurekodi muziki nchini, Inadaiwa kuwepo wimbo wa wasanii wawili waliowahi kuimba pamoja na wimbo wao ukawa gumzo kwa mashabiki wa muziki kipindi cha nyuma, wasanii hao wapo studio wakimalizia kurekodi nyimbo nyingine inayodaiwa kumzungumzia mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006.

No comments: