Thursday, 15 October 2015

Blatter:'Hakuna ushahidi wa kunishtaki'.

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter
Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ameripotiwa akisema kuwa anashtumiwa bila ushahidi wa makosa aliyofanya.
Matamshi yake yanajiri wakati alipoitwa 'mnafiki na muongo' na Chung Mong-Joon ambaye anapanga kumshataki raia huyo wa Uswizi kwa ubadhirifu wa fedha huku vilevile akitaka kumrithi katika FIFA.
Blatter anakabiliwa na uchunguzi kwa tuhuma za kutekeleza uhalifu wakati wa uongozi wake katika FIFA.
'Hakuna mashtaka',raia huyo mwenye umri wa miaka 79 aliliambia jarida moja la Ujerumani Bunte.
Chung Mong-Joon
 Chanzo-BBC.

No comments: