Wednesday, 14 October 2015

TUME YA UCHAGUZI YAWAKATA RAIA MIL,1 WASIO NA SIFA YA KUSHIRIKI UCHAGUZI 2015.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi{NEC},Jaji Damian Lubuva.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi , imeyaondoa majina ya wapiga kura zaidi ya milioni moja kutoka katika orodha ya awali ya watu milioni 23.7 waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura. Hii inatokana na kukamilika kwa kazi ya uhakiki wa majina ya watu wote waliojiandikisha. baada ya uhakiki, imebainika kuwa majina 1,031,769 kutoka miongoni mwa orodha ya awali hawastahili kuwamo kwani baadhi yao ni majina ya watu waliojiandikisha zaidi ya mara moja, wengine siyo Watanzania na wapo pia waliokosa sifa nyingine muhimu za kupiga kura, kwa mujibu wa sheria za nchi. Kwa sababu hiyo, Jaji Lubuva alisema idadi halisi ya watu watakaokuwa na fursa ya kupiga kura Oktoba 25 ni 22,251,292 kwa Tanzania Bara na wengine 503,193 wa visiwani Zanzibar.

Chanzo-EATV

No comments: