Thursday, 15 October 2015

WIMBO WA JAY Z WAZAMANI WAMPELEKA MAHAKANI.


Mmiliki wa Lebo ya Muziki nchini Marekani ya "Roc Nation" Jay z na Top ‘producer’ "Timbaland", jana walihudhuria mahakamani kujibu mashtaka ya kutumia ‘Biti’ ya mtu mwingine bila ya kupata ruhusa yake.
Kesi hii inahusisha ngoma ya Jay z iliyofanya vizuri sokoni mwaka 1999 ‘Big Pimpn’, mkwaju huo ulitengenezwa na Timbaland na biti yake ilichukuliwa kutoka kwa msanii  Mwenye asili ya Misri Baligh Hamdi, ambayo mwanzo aliita Khosara Khosara.
Kwa mujibu wa maelezo ya Timbaland, anasema alimlipa Hamdi kiasi cha dola laki moja kama malipo kabla ya kuitumia.
Sasa Timbwili hili jipya limeanzishwa na binamu wa Hamdi aitwae Osama Ahmed, ambaye amedai nae alihusika katika kuunda ‘dundo’ hilo.
Osama ametumia sheria za Misri zinazohusu pia maadili, na anauhakika wa kushinda.

NB:-Waweza Kuiangalia VIDEO ya NGOMA hiyo Hapo Chini,

No comments: