Monday, 16 November 2015

OLE MEDEYE KUGOMBEA USPIKA KUPITIA UKAWA.

Goodluck Ole Medeye
Wakati mchakato wa kumpata mwakilishi atakayewakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Uspika ukiendelea, imebainika kuwa Goodluck Ole Medeye , ndiye atakayesimama katika nafasi hiyo.
Ole Medeye, Mbunge wa Arumeru Magharibi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliwahi pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi katika utawala wa awamu ya nne wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), imeelezwa ndiye atakayewania nafasi hiyo.
Akizungumza , Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari, alisema hadi jana, mgombea pekee aliyekuwa anamfahamu ameshatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo, alikuwa ni Ole Medeye.

No comments: